Breaking News | Yaliyotabiriwa Yatimia Penzi la Diamond na Zuchu, Babu Tale Atoa Tamko
Diamond Platnumz; ni supastaa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye ni mmiliki wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye hatimaye yale yaliyotabiriwa kuwa hawezi kumuoa msanii wake, Zuchu, yametimia.
Yaliyotabiriwa Yatimia Penzi la Diamond na Zuchu, Babu Tale Atoa Tamko
Ikumbukwe kuwa, kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa, Diamond na Zuchu ni wapenzi kutokana na ishara za mahaba wanazozionesha, lakini jamaa huyp amesema kwamba, hawezi kumuoa mrembo huyo kwa sababu ni msanii wake.
Kauli ya Diamond au Mondi inakuja baada ya mmoja wa mameneja wake, Babu Tale kumwambia aoe kufuatia kuposti video akibusiana mdomoni na Zuchu.
“Sasa nitamuoaje wakati ni msanii wangu bosi, hilo busu hapo lisiwatishe viongozi, ni salamu tu za Kijerumani,” amesema Diamond.
Supastaa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz
Kama utakumbuka, Diamond na Zuchu ambao wametoa pamoja ngoma tatu, Litawachoma, Cheche na Mtasubiri, wamekuwa wakidaiwa kuwa ni wapenzi, lakini sasa ni wazi kuwa hakuna jambo kama hilo.
Post Comment
No comments