Subscribe Us

ads header

Breaking News

Ijue Nguvu ya Tabasamu Katika Maisha Yako




Ijue nguvu ya tabasamu

WANASAIKOLOJIA wa zamani na wa sasa wanakubali kwamba kuna zaidi ya aina 15 za tabasamu, zote zikitoa ujumbe tofauti. Mara nyingi hujulikana kama “the chosen vehicle for all ambiguities,” kutabasamu kunaweza kuonyesha woga, aibu, huzuni, au hata hasira.



Unajisikia vizuri unapotabasamu.

Kutabasamu huongeza homoni zinazoongeza hisia huku kikipunguza homoni zinazoongeza mfadhaiko, zikiwemo cortisol na adrenaline. Pia hupunguza shinikizo la damu kwa ujumla. Na kwa sababu kwa kawaida unatabasamu ukiwa na furaha, misuli inayotumiwa huchochea ubongo wako kuongeza endorphins ambayo ni kemikali inayoondoa maumivu na hasira.



Kutabasamu kunaweza kukusaidia kuishi maisha marefu zaidi.

Kulingana tafiti zilizofanywa na chuo kikuu Havard katika kada ya afya inaeleza, matumaini ambayo mtu hupata yanahusishwa na kutabasamu hupelekea hupunguza athari ya kifo na maambukizi. Na kulingana na utafiti katika jarida lililokaguliwa na wenzao Proceedings of the National Academy of Science, watu wanaopata matumaini ya juu zaidi wana muda mrefu zaidi wa maisha.



Huongeza siku za kuishi

Hata pia kutabasamu kunaweza kuwa na sura tofauti juu ya jinsi unavyochukuliwa.Kulingana na uchunguzi uliofanywa kuchunguza mvuto wa kimapenzi wa watu kulingana na kuonesha furaha, kwa wanaume ilibainika tabasamu lilikuwa ni mvuto mkali wa hisia kwa mwanamke; kwa wanawake,tabasamu lilikuwa ni mvuto wa kawaida kwa hisia kwa mwanaume . Mwisho ilikuja kubainishwa kuwa tabasamu huleta hisia tofauti za kimapenzi kulingana na jinsia.



Kutabasamu sio tabia ya kujifunza.

Amini usiamini, wanadamu tumezaliwa tukiwa tunatabasamu. Pamoja na maendeleo ya teknolojia madaktari na matibabu wameweza kutambua kwamba watoto hutabasamu wakiwa tumboni mwa mama na huendelea kutabasamu hata wanapozaliwa. Hii ni kweli kwa watoto wote bila kujali tamaduni na mazingira, kwani kutabasamu ni hali ya kibaolojia wa kibinadamu.



Watoto hutabasamu wakiwa tumboni mwa mama

No comments