Subscribe Us

ads header

Breaking News

Vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo | Your Guide to University Life


Hongera kwa kufika chuo tena, sehemu yenye uhuru na maamuzi unayoyafanya mwenyewe. Hakuna kitu kizuri kama hicho kwenye maisha, kuwa huru. Katika yote chuo, leo ningependa kukuambia vitu 5 vya kuwa navyo makini unapokuwa chuo, vya kuviangalia kwa jicho la tofauti maana vina umuhimu kwenye maisha yako ya chuo. Vitu vyenyewe ni:
Kitu cha 1: Urafiki utakaouchagua
Kuna msemo unasema “nionyeshe marafiki zako watano, nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani”, lakini pia watu husema, marafiki utakao watengeneza chuo unaweza kudumu nao mpaka milele”, inawezekana ni kweli au sio kweli lakini ninakubaliana nao. Chuoni ni sehemu ambako nimetengeneza urafiki, tena wa kweli. Kuwa makini na kuchagua marafiki wako hasa sasa. Watu utakaowapata chuo wanaweza kukusababisha ufanikiwe au usifanikiwe kwenye maisha kwahiyo kuwa makini na chaguzi yako.
Kitu cha 2: Masomo yako
Kuna watu wanasema GPA haina umuhimu, inawezekana ni kweli au si kweli, lakini kumbuka sababu kuu iliyokupeleka chuo ni kusoma, kwahivyo kuwa makini na masomo yako, ni heri kuona GPA haina umuhimu ukiwa nayo nzuri, kuliko usipokuwa nayo nzuri. Mimi nimepata cheti changu but from to time nikikiangalia I wish niongeze point 0.1 tu ili nibadilishe class kabisa. You don’t have to live like me??
Kitu cha 3: Matumizi ya hela
Hivi karibuni nimepiga mahesabu ya hela nilizokuwa nazipata nikiwa chuoni, na nikagundua kuwa kama ningekuwa mtumiaji mzuri ningekuwa hata bilionea (au hata milionea basi??), lakini sikuwa na huo ufahamu au hata sikupewa ushauri basi toka naanza chuo. Lakini sitaki wewe upitie njia hiyohiyo, maana unaweza ukakosa hata nauli ya kusambazia hiyo barua ya kuombea kazi ukimaliza chuo.
Unaweza ukawa na matumizi mazuri ya hela ukiwa chuoni kwa:
-Kuwa na budget ya matumizi ya hela zako (hili nitaliongelea kwenye post zijazo)
-Kufungua biashara ambazo zitakuingizia kipato (saloon na biashara ya chakula ni biashara maarufu sana maeneo ya chuo)
– Kukaa na marafiki zako sehemu moja ili kusave hela
-Kufungua savings account au fixed account kwaajili ya pesa zako. Saving account usiiiguse kabisa utahifadhi tu hela, na fixed itakusaidia kuongeza hela baada ya kuiacha kwa muda.
-Kuweka bill (mimi sikuweka bill, ila walioweka bill wanasema iliwapunguzia gharama za maisha)
Kitu cha 4: Afya yako
Kuwa makini na afya yako labda ningeweka kama kitu cha kwanza kwasababu chuoni unapitia/utapitia vingi sana vitakavyokuletea stress kwenye maisha yako hapo chuo, kumbuka unadeal na masomo lakini wakati huohuo kuna familia inakuzunguka, mahusiano, drama za marafiki, lakini siku nyingine unakuwa tu umechoka, kuwa makini na afya yako, kwasababu hakuna umuhimu wa wewe kuugua au kupata matatizo eti kisa unasoma sana, na hata hivyo ukiugua hauwezi hata kusoma. Hivyo kuwa makini na afya yako, physically, emotionally, spiritually, socially na psychologically.
Unaweza kufanya mambo yafuatayo katika kukusaidia kuwa makini na afya yako:
-Kufanya mazoezi
-Kunywa maji, kula vizuri,kupumzika muda wa kutosha( masaa nane)
-Kutoka nje ya mazingira ya chuo, kutembelea vivutio,beach nk
-Kukutana na marafiki, hakikisha una mtu hata mmoja unaemuamini kushirikiana naye unapopitia matatizo.
Kitu cha 5: Image yako
Kuwa makini sana na image yako unapokuwa chuoni. Siri moja katika maisha ni kwamba hakuna watu wapya( zaidi ya waliozaliwa), hao uliotoka nao primary wengine mnakutana chuo au mtakutana ofisini au uliokutana nao chuo watakutana ofisini na watu uliosoma nao primary, kwahiyo kuwa makini na image yako unayoiweka mbele za watu. Okay, hapa simaanishi uigize maisha ya watu ambayo siyo yako, na simaanishi ubadilishe maisha yako ili uonekane perfect, namaanisha maisha yenye taarifa mbaya, au image mbaya ambayo watu wataipata kuhusu wewe.
Na hivyo ni vitu vitano vya kuzingatia unapokuwa chuo. Ila kikubwa zaidi ya vyote, ni usimuache Mungu, alikusaidia huku chini, atakusaidia na chuo pia

No comments