Subscribe Us

ads header

Breaking News

HARMONIZE MATATIZO LYLICS


Haiyee aaah! Olelelelee

Alfajiri imefika Anga inang'aa Mvua inaanza katika Ghafla tumbo la njaa

Naweka sauti kwa spika Nipate umbea wa dar

Mara simu inaita Jina la anko Twaha…Akisema,

Mama yu hoi kitandani Kama si wa leo wa kesho

Na kupona sizani Upate japo neno la mwisho

Mi ndo mtoto wa pekee Nyumbani wananitegemea Mdogo wangu wa kike

Hali duni alishagaolewa

Tizama jasho langu la mnyonge Kipato hakikidhi mahitaji Napiga moyo konde

Yarabi mola ndo mpaji

Matatizo, matatizo Yatakeisha lini Matatizo Kila siku mimi

Ewe mola Matatizo yatakwisha lini Japo likizo Nifurahi na mimi

Mola aliniumba na subira Imani pekee ngao yangu Mbona nishasali sana Ila mambo bado tafarani

Mama kanifunza kikabila Nikonde sana haini yangu Tena nijitume sana Na vya watu nisivitamani

Hata mpenzi niliyenae Najua siku atanikimbia Itanitesa ye ndo nguzo

Zile ngoja kesho badae Atazichoka kuzivumilia Anakosa hata matunzo

Ona, nadaiwa kodi nilipopanga Nashinda road nikihanda Nishapiga hodi kwa waganga

Kwa kuhisi narogwa

Nikauza maji na karanga Nikawa dobi kwa viwanda Ila kote ziro ni majanga

Mtindo mmoja

Mi ndo mtoto wa pekee Nyumbani wananitegemea Mdogo wangu wa kike

Hali duni alishagaolewa

Tizama jasho langu la mnyonge Kipato hakikidhi mahitaji Napiga moyo konde

Yarabi mola ndo mpaji

Matatizo, matatizo Yatakeisha lini (ewe mola) Matatizo Kila siku mimi (jamani matatizo)

Matatizo, (oh matatizo) Yatakeisha lini Japo likizo Nifurahi na mimi (iih matati...)

Matatizo (matati...) Yatakeisha lini Matatizo Kila siku mimi (jama matatizo)

Matatizo, matatizo Yataisha lini (ye iye)

No comments