Subscribe Us

ads header

Breaking News

Huzuni | Mama alinioza kwa 'sponsor' wake ili apate pesa- Mwanamke asimulia | Sorrow | My mother married me to her 'sponsor' in order to get money - The woman does not tell

Nilipoanza kupika chang'aa mama pia alinilazimisha nianze kubuga pombe, kwani aliniuliza naweza aje pika chakula bila kukionja."

Muhtasari
Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na Kendi ambaye alinisimulia jinsi mama yake alimuoza kwa sponsor huku akifundisha kazi ya ukahaba


sad woman


Maiha ya uotoni kwake Kendi hayakuwa ya kawaida au ya kufurahisha kama ya watoto wengine, wanavyofurahia wakiwa na wazazi wao.

Kulingana na Kendi, maisha yake yaliharibiwa na mama yake mzazi, kwani alimuoza kwa 'sponsor' wake akiwa darasa la nne.

Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na Kendi ambaye alinisimulia jinsi mama yake alimuoza kwa sponsor huku akifundisha kazi ya ukahaba.



Je nini kilichosababisha Kendi kuozwa?

"Mama yangu alikuwwa kahaba nilipokuwa mtoto mdogo kwani niliishi naye na kushuhudia akiwaleta wanaume tofauti nyumbani kwake

Wakati huo nilikuwa darasa la nane, mmoja wa wanaume wake alinisaidia na pesa ili nunue penseli, kwani mama yangu alikuwa amekataa na kuniambia kwamba amechoka kunisomesha

Hapo ndipo mwanamume huyo alianza kunitongoza na kisha tukafanya ngono naye na kubeba ujauzito."

Aliongeza;

"Mama aligundua kwamba nina ujauzito na nikamwambia mwenye ujauzito ni nani, baada ya kujifungua alinioza kwa sponsor wake ambaye alikuwa akifanya ngono a mama yangu anarudi anafanya ngono na mimi

Baada ya muda mama alinifungulia biashara ya kuuza chang'aa, hapo ndipo masomo yangu yalifika mwisho,uchungu ambao nimeishi nao kwa zaidi ya miaka 30 ni kwa ajili ya amama yangu, hata baada ya kujua kwamba amekosa na kuharibu maisha yangu hakuweza kuniomba msamaha



Nilipoanza kupika chang'aa mama pia alinilazimisha nianze kubuga pombe, kwani aliniuliza naweza aje pika chakula bila kukionja."

No comments