Subscribe Us

ads header

Breaking News

Najuta kurudiana na mke wangu, baada ya kuniacha kwa miezi 6-Mwanamume afichua siri | I regret getting back together with my wife, after leaving me for 6 months - The man reveals a secret

Muhtasari
Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na Muema ambaye alinisimulia jinsi alivoachana na mke wake na kisha wakarudiana baada ya miezi 6

black-woman-crying-


Ni mienendo na tabia ambazo wanandoa wa sasa wamejifunza, kuachana na kisha kurudiana baada ya muda.

Lakini sababu ya wanandoa wengi kufanya haya ni nini?

Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na Muema ambaye alinisimulia jinsi alivoachana na mke wake na kisha wakarudiana baada ya miezi 6.


Lakini swali kuu kwake, ni kwa nini wanafanya hayo,kwa mujibu wwake alisema kwamba kila mwenzi anajiona kwamba yeye ndio kujua, na kuona kuwa wote ni vichwa vya familia.

Katika biblia mwanamume ndiye kichwa cha nyumba na mwanamke ndiye shingo,, lakini sio kwwa wanandoa wa sasa.

Muema anajuta kurudiana na mkewe kwani kwa sasa analea mtoto ambaye ni wa mwanamume mwingi, na zaidi ya yote mkewe alimuambukiza virusi vya ukimwa.
Huu hapa usimulizi wake;

"Ningeambiwa niache mke wangu sikuza kwanza katika ndoa yetu singekubali wala kufikiria kumuacha mwanamkewangu, baada ya kubarikiwa na mtoto mmoja mke wangu alibadilika baada ya miaka 3kisha akaniacha

Kweli niona ni kama naota lakini hayo ndio yalikuwa mambo na changamoto za maisha yangu, kwa kweli nilimpenda na kwani baada ya miezi 6 alirudi na kumpokea na mikono yote

Najuta sana kurudiana naye kwani aliniambukiza virusi vya ukimwi bila yangu kujua, sasa nina miaka 15 nikiishi na ugonjwa huo laakini namshukuru Mungu kwani nimekuwa nikinywa dawa na niko hai na waona wanagu wanakuwa na kunipa tabasamu moyoni na usoni ata licha yangu kuwa na mauamivu.

Kwa kweli mwanamke huyo aliniacha na maumivu ya mwili na rohoni," Alisimulia.

No comments