Phiri, Okrah waahidi makubwa Dabi ya kariakoo, Yanga na simba

ACHANA na ushindi walioupata Simba dhidi ya Primeiro de Agosto na kuwavusha hatua ya makundi, unaambiwa kikosi hicho kwa sasa akili zao wamezielekeza mechi dhidi ya Yanga itakayopigwa Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa.
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kutokana na upinzani ulipo baina ya miamba hii kwa sababu ya historia zao, huku kila mmoja akitaka kushinda ili kuwafurahisha mashabiki na kulinda heshima yake isishuke kirahisi.
Nyota wa kikosi hicho, Augustine Okrah alisema sio mechi rahisi kutokana na upinzani uliopo ingawa matokeo yao yaliyopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yamewapa nguvu hivyo wana imani kubwa ya kuibuka na ushindi.
Post Comment
No comments