Rais Samia ataka Watanzania kupunguza kasi ya kuzaa | President Samia wants Tanzanians to reduce the rate of childbirth
Samia amewataka wananchi kupunguza kasi ya kuzaa kutokana ongezeko la idadi ya watoto wanaozaliwa kwa sasa.
Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Image: GOOGLE
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wake kupunguza kasi ya kuzaa, kutokana ongezeko la idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kwa sasa.
Ametoa kauli hiyo baada ya kushtushwa na taarifa aliyopewa kuhusu idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kwa mwezi.
Akizungumza na wananchi hao wa Bukombe, magharibi mwa Tanzania, Rais Samia alitoa kauli hiyo akiwata wapunguze kasi.
''Jana nimesimama Buselesele pale, nikaambiwa kituo kimoja (cha afya) kinazalisha watoto 1,000 kwa mwezi, sasa hayo madarasa baada ya miaka 3 ni mangapi?, kama ni vituo vya afya ni vingapi? tani za chakula ni ngapi,? kidogo speed (kasi) tupunguze kidogo'', alisema rais Samia.
Rais Samia aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kawaida ya kiserikali ndani ya nchi hiyo.
Katika kiwango cha sasa cha ukuaji wa idadi ya watu, idadi ya watu huongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka 25.
Wakati ikisubiriwa taarifa rasmi ya sensa ya watu iliyofanyika mwaka huu, nchi hiyo inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 60, kutoka kadirio la watu milioni12.5, katika miaka ya 1960.
No comments